Burkina Faso Yapitisha Sheria Kali Dhidi ya Mapenzi ya Jinsia Moja
Tarehe 1 Septemba 2025, bunge la mpito la Burkina Faso limeidhinisha sheria inayopiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja. Sheria hii mpya inahusisha adhabu ya kifungo cha miaka 2 hadi 5 na faini kubwa kwa wahusika.
Waziri wa Sheria, Edasso Rodrigue Bayala, alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda maadili ya familia. Sheria pia inaruhusu kufukuzwa kwa raia wa kigeni wanaopatikana na hatia ya vitendo hivyo.
Makundi ya haki za binadamu kama Amnesty International na Human Rights Watch yamekosoa vikali sheria hiyo, wakisema inakiuka haki za msingi za binadamu na inachochea chuki dhidi ya watu wa LGBTQ+.
Burkina Faso sasa imejiunga na orodha ya zaidi ya nchi 30 barani Afrika zinazopiga marufuku mahusiano ya jinsia moja, ikifuata nyayo za Ghana, Uganda, na Mali.
by Twaha Ahmadi | Iliandikwa 03/09/2025
