Kwa mujibu wa vyanzo vya Israeli, serikali ya Hispania inadaiwa kufuta au kusitisha baadhi ya mikataba ya ununuzi wa silaha kutoka kwa makampuni ya Israeli, yenye thamani ya takriban €300 milioni. Hatua hii inatajwa na wachambuzi kama mojawapo ya msimamo mkali zaidi barani Ulaya dhidi ya Israel tangu kuanza kwa vita ya Gaza mnamo Oktoba 2023. Mikataba inayodaiwa kuathiriwa ni pamoja na mfumo wa makombora ya PULS kutoka Elbit Systems, makombora ya Spike LR 2 kutoka Rafael, na risasi milioni 15 kwa ajili ya Civil Guard. Vyama vya mrengo wa kushoto ndani ya serikali ya muungano vilipinga vikali ununuzi huo, wakisema ni kinyume na misingi ya haki za binadamu. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi na mamlaka za Hispania. Kwa taarifa zaidi kuhusu hatua za kimataifa na athari zake kwa Mashariki ya Kati.
by Twaha Ahmadi | 15/09/2025