Rais Évariste Ndayishimiye akivuna nyanya kwenye shamba la mfano lililopo Shombo, Gitega

Tarehe 12 Septemba 2025, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye, alifanya ziara ya kutembelea miradi ya kilimo ya kisasa katika kijiji cha Nyarurambi, kilichopo katika commune ya Shombo, mkoani Gitega. Akiwa huko, alitembelea shamba la parachichi aina ya HASS lenye zaidi ya miti 15,000, lililopandwa kwenye eneo la ekari 11 na kumilikiwa na mkulima kijana, Kwizera Elias. Aidha, Rais Ndayishimiye alielekea kwenye kijiji cha Mugogo, pia ndani ya Shombo, kwa ziara ya kumtia moyo Mheshimiwa Serge Ndayisenga, mkulima wa mfano anayelima kisasa zaidi ya ekari 35 za viazi na mahindi, akishirikiana na vikundi vya wanawake wa vijijini. Kwa kuonyesha mfano wa vitendo, Rais Ndayishimiye na Mkewe, Mama Angeline Ndayishimiye, walivuna nyanya kutoka kwenye shamba lao la mfano lililopandwa ndani ya greenhouse ya mita za mraba 90, kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji wa matone. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha kati ya tani 5 hadi 6 za nyanya. Wanandoa hao wa Ikulu pia walitembelea shamba lao la kabichi lililopandwa ndani ya greenhouse. Miradi hii ni sehemu ya kampeni ya Rais Ndayishimiye ya kuhamasisha wananchi kutumia mbinu za kisasa za kilimo zenye tija kubwa hata kwenye maeneo madogo, kwa msimu wowote wa mwaka. Kwa taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya kilimo na juhudi za viongozi wa Afrika Mashariki.

picha-ndogo-ya-mwandishi by Twaha Ahmadi | 15/09/2025

← Rudi Mwanzo Toa Maoni

Shiriki habari hii: