Mnamo tarehe 9 Septemba 2025, ndege za kivita za Israel zilitekeleza shambulio la anga dhidi ya viongozi wa Hamas waliokuwa kwenye kikao cha kisiasa mjini Doha, Qatar. Kwa mujibu wa ripoti ya [Firstpost] maafisa wa Israel wamedai kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alimjulisha Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu operesheni hiyo dakika 50 kabla ya makombora kurushwa.
Hata hivyo, Trump amekanusha madai hayo akisema hakufahamishwa mapema, na kwamba alijulishwa na jeshi la Marekani wakati mashambulizi yalikuwa tayari yameanza. Shambulio hilo liliwaua wanachama watano wa Hamas na afisa mmoja wa usalama wa Qatar, huku viongozi wakuu wa Hamas wakinusurika baada ya kuondoka kwenye jengo hilo muda mfupi kabla ya mashambulizi. Tukio hili limezua mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Israel, Marekani, na Qatar, na limeathiri mazungumzo ya kusitisha vita vya Gaza vilivyodumu kwa takriban miaka miwili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani shambulio hilo akilitaja kama "ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Qatar.
by Twaha Ahmadi | 15/09/2025
